Ubishi - Komaa na Maisha
"Nguvu kuu ni uelewa. Uelewa wa mapito yanayojiri katika maisha kwa kuzingatia mambo ya msingi yanayotuunganisha sisi wanadamu ni dawa tosha.
Usidanganyike. Kipimo cha maisha sio tu kufanikiwa. Kipimo cha maisha sio tu kushindwa. Kipimo hasa cha maisha ni uwezo wa mtu kustahimili mapambano yanayojiri kati ya kufanikiwa na kushindwa.
Haitoshi kuhamasika na picha ya mafanikio ama kuogopa piclaa ya kushindwa kama hauwekezi kwenye roho ya mapambano ambayo asili yake inatokana na ujana wako ama tabia ubishi. Soma kitabu hiki upate lisheya roho ili uwezo kuimarika katika mapambano yako"
Costantine Magavilla ama Mwalimu Kifimbo ni mshauri elekezi na mzungumzaji katika maswala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya watu na jamii, usimamizi wa biashara na masoko na pia ni mtayarishaji mahiri wa maonyesho ya sanaa (maigizo na matamasha) na biashara, mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini ndani na nje ya nchi. Ni mtunzi wa kitabu cha kwanza cha aina yake kwenye tasnia ya uhamasishaji fikra chanya Nchini na Afrika Mashariki kiitwacho "Life and You - a journey through self” mwaka 2007.
Magavilla anapenda kujinasibisha na utumbuaji fikra potofu na kuhamasisha watu kuyaelewa yanayojiri katika mazingira yao kwa kuzingatia mambo ya msingi na sio tu nguvu ya matukio. Ameshauri watu wengi kuanzia wana siasa, wana harakati, wafanyabiashara, wasanii, vijana wa mtaani, wanafunzi hadi wafanyakazi kotoka ngazi zote kwa mafanikio makubwa sana.