Ubishi - Komaa na Maisha
"Nguvu kuu ni uelewa. Uelewa wa mapito yanayojiri katika maisha kwa kuzingatia mambo ya msingi yanayotuunganisha sisi wanadamu ni dawa tosha. Usidanganyike. Kipimo cha maisha sio tu kufanikiwa. Kipimo cha maisha sio tu kushindwa. Kipimo hasa cha maisha ni uwezo wa mtu kustahimili mapambano yanayojiri kati ya kufanikiwa na kushindwa. Haitoshi kuhamasika na picha ya mafanikio ama kuogopa piclaa ya kushindwa kama hauwekezi kwenye roho ya mapambano ambayo asili yake inatokana na ujana wako ama tabia ubishi. Soma kitabu hiki upate lisheya roho ili uwezo kuimarika katika mapambano…